Mark 15:20-25

20 aWalipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulubishe.

Kusulubiwa Kwa Isa

(Mathayo 27:32-44; Luka 23:26-43; Yohana 19:17-27)

21 bMtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Iskanda na Rufo, alikuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shamba, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. 22 cKisha wakampeleka Isa mpaka mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). 23 dNao wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini hakuinywa. 24 eBasi wakamsulubisha, nazo nguo zake wakagawana miongoni mwao kwa kuzipigia kura ili kuamua ni gani kila mtu ataichukua.

25 fIlikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha.
Copyright information for SwhKC